Watu wanane wamekufa katika mlipuko Misri
Zaidi ya watu WANANE wamekufa nchini MISRI katika mlipuko baada ya watu kujitoa mhanga kwa kutega bomu kwenye gari Kaskazini mwa mji wa SINAI.
Masalia ya shambulizi la bomu la kujitoa mhanga, Cairo - Misri

Zaidi ya watu WANANE wamekufa nchini MISRI katika mlipuko baada ya watu kujitoa mhanga kwa kutega bomu kwenye gari Kaskazini mwa mji wa SINAI.

 

Taarifa zinasema mtu aliyejitoa mhanga alijilipua katika kituo cha ukaguzi karibu na jengo moja huko EL –ARISH akiwa kwenye lori lililojaa vilipuzi.

 

Mpaka sasa hakuna kundi lililokiri kuhusika na milipuko hiyo ingawa eneo hilo limekuwa likilenga mara kadhaa na kundi la wanamgambo wenye mshikamano na kundi la ISLAMIC STATE.

 

Kundi hilo la IS linaaminika kwamba limeishafanya mashambulizo zaidi ya 400 Kaskazini mwa SINAI kati ya mwaka 2012 na 2015.

 

 

JUDICA LOSAI

JANUARI 09, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI