Baridi kali yaua watu ishirini barani ULAYA
Watu ISHIRINI wamekufa barani ULAYA kutokana na baridi kali. Hali ya hewa ya baridi kupita kiasi imekuwa chanzo cha vifo vinavyotokea katika nchi za Mashariki na katikati mwa bara la ULAYA.
Baridi kali nchini Poland

Watu ISHIRINI wamekufa barani ULAYA kutokana na baridi kali. Hali ya hewa ya baridi kupita kiasi imekuwa chanzo cha vifo vinavyotokea katika nchi za Mashariki na katikati mwa bara la ULAYA.

Nchi ya UKRAINE joto limeshuka mpaka kipimo cha joto hasi 25 ambapo barabara zote zimetanda theluji. Huko ISTANBUL theluji imejaa katika viwanja vya ndege na kusababisha safarai za ndege 600 kuhairishwa.

Nchini ROMANIA watu WANNE wamepoteza maisha kutokana na baridi kali. Taarifa zinasema watu wako kwenye hatari kubwa ya kupoteza maisha katika kambi za wakimbizi.

JUDICA LOSAI

JANUARI 09, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI