IRAN yaanza maombolezo ya kifo cha AKBAR HASHEMI RAFSANJANI
IRAN imeanza siku TATU za maombolezo kufuatia kifo cha rais wa zamani wa nchi hiyo AKBAR HASHEMI RAFSANJANI aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82.
Rais wa zamani wa IRAN, AKBAR HASHEMI RAFSANJANI amefariki akiwa na umri wa miaka 82.

IRAN imeanza siku TATU za maombolezo kufuatia kifo cha rais wa zamani wa nchi hiyo AKBAR HASHEMI RAFSANJANI  aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82.

RAFSANJANI aliongoza IRAN kwa miaka NANE kati ya mwaka 1989 mpaka 1997 na baadaye kuendelea kushika nyasifa mbalimbali nchini humo.

Kiongozi wa kidini wa IRAN, AYATOLLAH  ALI KHAMENEI ametoa  salamu za rambirambi kufuatia kifo cha aliyekuwa rais wa nchi hiyo na kusema atakumbukwa daima katika historia ya nchi ya IRAN.

Maelfu ya waombelezaji wamekusanyika kutoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi wao. Mazishi ya RAFSANJANI yatafanyika kesho.

JUDICA LOSAI

JANUARI 09,2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI