Waziri mkuu IVORY COAST ajiuzulu
Waziri mkuu wa IVORY COAST, DANIEL KABLAN DUNCAN amejiuzulu na kuvunja baraza la mawaziri ikiwa ni njia ya kufuatilia kuidhinishwa kwa katiba mpya na uchaguzi wa ubunge wa mwezi uliopita.
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa IVORY COAST, DANIEL KABLAN DUNCAN

Waziri Mkuu wa IVORY COAST, DANIEL KABLAN DUNCAN amejiuzulu na kuvunja baraza la mawaziri ikiwa ni njia ya kufuatilia kuidhinishwa kwa katiba mpya na uchaguzi wa ubunge wa mwezi uliopita.

 

Waziri mkuu DUNCAN amesema amekabithi barua  yake ya kujiuzulu ofisini baada kukutana na rais ALASSANE QUATTARA ambaye anatarajiwa kuvunja baraza la mawaziri kufuatia mapigano yaliyotokea nchini humo Ijumaa wiki iliyopita wanajeshi wakidai nyongeza ya mishahara.

 

Awali upinzani ulisusia Uchaguzi wa ubunge miaka 5 iliyopita, kufuatia machafuko ya kisiasa yaliyodumu miezi kadhaa, na kupelekea vifo vya watu ELFU TATU.

 

 

JUDICA LOSAI

JANUARI 09, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI