Huduma za usafiri wa ndege zarejea Fort Lauderdale
Huduma za usafiri wa ndege zimerejea katika uwanja wa ndege wa Fort Lauderdale baada vyombo vya usalama vya MAREKANI kumkamata kijana aliyehusika na mauaji uwanjani hapo.
Abiria wakisubiri huduma ya usafiri katika uwanja wa ndege wa Fort Lauderdale jumapili tarehe 07/01/2017 kufuatia tukio la mauaji uwanjani hapo. Huduma ya usafiri katika uwanja huo imerudi katika hali ya kawaida.

Huduma za usafiri wa ndege zimerejea katika uwanja wa ndege wa Fort Lauderdale baada vyombo vya usalama vya MAREKANI kumkamata kijana aliyehusika na mauaji uwanjani hapo.

 

Maafisa wa Marekani wanachunguza sababu iliyomfanya mwanajeshi wa zamani kuuwa watu WATANO  na kuwajeruhi wengine WANANE baada ya kuwafyatulia risasi katika uwanja huo wa ndege huko FLORIDA.

 

ESTEBAN SANTIAGO mwenye umri wa miaka 26 ambaye alikuwa mlinzi nchini IRAQ kabla ya kuondolewa na kuachishwa kazi mwaka jana ndiye aliyehusika na mauaji hayo.

 

Ndugu yake amesema katika siku za hivi karibuni alikuwa anatibiwa kwa matatizo ya akili. 

 

 

JUDICA LOSAI

JANUARI 07, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI