Rais wa Ghana aapishwa
NANA AKUFO ADDO ameapishwa leo kuwa rais wa GHANA baada ya kumshinda Rais JOHN MAHAMA katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo Decemba 2016.
NANA AKUFO ADDO akila kiapo kuwa rais wa GHANA

NANA AKUFO  ADDO ameapishwa leo kuwa rais wa GHANA baada ya kumshinda Rais JOHN MAHAMA katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo Decemba 2016.

 

Sherehe za kuapishwa kwake zimefanyika katika viwanja vya uhuru katikati ya mji mkuu ACCRA na kuhudhuriwa na viongozi wa nchi KUMI na MOJA za AFRIKA na maelfu ya raia wa GHANA.

 

Viongozi wa zamani wa GHANA akiwepo JOHN MAHAMA, JOHN RAWLINGS na JOHN KUFUOR wamehudhuria sherehe hizo za kuapishwa kwa rais ADDO.

 

ADDO mwenye umri wa miaka 72 anayeongoza chama cha New Patriotic amewahi kuwa wakili wa haki za binadamu na amegombea nafasi ya urais mara MBILI nakufanikiwa kushinda mara hii ya TATU.

 

Baada kuapishwa kwa ADDO viongozi  wa AFRIKA waliohudhuria sherehe hiyo watajadili namna ya kuhakikisha kuwa Rais wa GAMBIA, YAHYA JAMMEH, anaondoka madarakani baada ya kukataa  kustaafu ingawa alishindwa katika uchaguzi wa Mwezi Disemba.

 

 

JUDICA LOSAI

JANUARI 07, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI