Cleveland Cavaliers waibuka washindi NBA
Ligi ya kulipwa ya mpira wa kikapu ya NBA nchini MAREKANI mabingwa watetezi CLEVELAND CAVALIERS wameibuka na ushindi wa alama 116 dhidi ya 108 za BROOKLYN NETS
Mchezaji wa mpira wa kikapu wa CLEVELAND CAVALIERS inayoshiriki ligi NBA, Kevin Love akichuana na mwezake wa timu ya kikapu inayoshifiki ligi ya NBA ya MAREKANI

Ligi ya kulipwa ya mpira wa kikapu ya NBA nchini MAREKANI mabingwa watetezi CLEVELAND CAVALIERS wameibuka na ushindi wa alama 116 dhidi ya 108 za BROOKLYN NETS katika mchezo ambao nyota wa CLEVELAND LEBRON JAMES alifunga alama 36 peke yake.

 

KYRIE IRVING nae akaipa chagizo la ushindi CLEVELEND kwa kufunga alama 32 katika ushindi huo.

 

Katika matokeo mengine HOUSTON  ROCKETS wamewanyuka  ORLANDO MAGIC  alama 100 kwa 93 huku mchezaji wao nyota JAMES HARDEN akifunga alama 14 na kutoa pasi 10 za ushindi.

 

Nao MEMPHIS  GRIZZLIES wamewatoa nishai GOLDEN STATE WARRIORS na kuwapa kipigo cha alama  128  kwa 119, MIAMI HEAT wakinyukwa alama 127 kwa 100 dhidi ya LOS ANGELES LAKERS na BOSTON CELTICS  wakishinda alama 110 kwa 106 za PHILADELPHIA.

 

 

ENOCK BWIGANE

JANUARI 07, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI