Jeshi la Polisi KENYA lapewa lawama
Baadhi ya ndugu na jamaa wa wanajeshi wa KENYA waliokufa katika shambulio lililotekelezwa na wapiganaji wa AL-SHABAB nchini SOMALIA wamelilalamikia Jeshi la KENYA kwa kutotoa taarifa sahihi kuhusiana na shambulio hilo.
Wanajeshi wa KENYA wakiwa na huzuni katika kuwakumbuka wenzao walioshambuliwa na wapiganaji wa AL-SHABAB nchini SOMALIA katika Kambi ya Jeshi kwenye Mji wa EL-ADE

Baadhi ya ndugu na jamaa wa wanajeshi wa KENYA waliokufa katika shambulio lililotekelezwa na wapiganaji wa AL-SHABAB nchini SOMALIA wamelilalamikia Jeshi la KENYA kwa kutotoa taarifa sahihi kuhusiana na shambulio hilo.

Ndugu hao wa wanajeshi wa KENYA wanaopigana na wapiganaji wa AL-SHABAB nchini SOMALIA wametoa malalamiko yao kufuatia ukimya wa Jeshi la KENYA kuhusu idadi halisi ya wanajeshi wake waliokufa katika shambulio lililotekelezwa Januari 15 mwaka huu na wapiganaji wa AL-SHABAB katika Kambi ya Jeshi kwenye Mji wa EL-ADE Kusini mwaSOMALIA.

Jeshi la KENYA linadai wanajeshi wake waliokufa katika shambulio hilo ni WANNE wakati wapiganaji wa AL-SHABAB pamoja na Rais  HASSAN SHEIKH MOHAMUD wa SOMALIA wakieleza kuwa zaidi ya wanajeshi MIA MBILI wameuawa katika shambulio hilo.

GHANIA JUMBE

DESEMBA 6, 2016

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI