Kamanda wa zamani wa LRA akanusha mashtaka yake ICC
Kamanda wa zamani wa kundi la waasi wa Lord's Resistance Army-LRA, DOMINIC ONGWEN amekanusha mashtaka dhidi yake mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai -ICC.
Kamanda wa zamani wa kundi la waasi wa Lord's Resistance Army-LRA la UGANDA, DOMINIC ONGWEN

Kamanda wa zamani wa kundi la waasi wa Lord's Resistance Army-LRA, DOMINIC ONGWEN amekanusha mashtaka dhidi yake mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai - ICC.

 

DOMINIC ONGWEN ameiambia mahakama hiyo iliyoko Mjini THE HAGUE nchini UHOLANZI kuwa, binafsi alitekwa nyara akiwa kijana na kulazimishwa kujiunga na harakati za wapiganaji wa msituni wa LRA mwishoni mwa miaka ya 80, huku akikanusha mashtaka 70 yanayomkabili, yakiwemo ya mauaji na udhalilishaji.

 

Majaji wa ICC awali walikataa ombi la mawakili wa ONGWEN, waliotaka mteja wao afanyiwe uchunguzi wa kiakili kabla ya kuanza kusikilizwa kesi hiyo.

 

Kundi la waasi la LRA lilianzisha harakati zake nchini UGANDA na baadaye likapanua wigo wa harakati hizo hadi katika nchi za SUDAN KUSINI, CHAD na hata katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

 

Umoja wa Mataifa unasema kundi la Lord's Resistance Army limeua zaidi ya watu LAKI MOJA na kuteka nyara watoto Elfu SITINI.

 

 

GHANIA JUMBE

DESEMBA 6, 2016

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI