​ KENYA kupokonya silaha maeneo ya mipakani
Serikali ya KENYA imetangaza inakusudia kutekeleza mpango wa upokonyaji silaha katika maeneo ya nchi hiyo yanayopakana na nchi za SOMALIA na ETHIOPIA.
Wakazi wa maeneo ya jirani na mipaka ya Somalia na Ethiopia nchini Kenya wametakiwa na Serikali kukabidhi kwa hiari silaha wanazomiliki kinyume cha sheria.

Serikali ya KENYA imetangaza inakusudia kutekeleza mpango wa upokonyaji silaha katika maeneo ya nchi hiyo yanayopakana na nchi za SOMALIA na ETHIOPIA.

 

Jeshi la Polisi nchini KENYA limewataka wakazi wa maeneo ya MANDERA, WAJIR na GARISSA yaliyoko jirani na mipaka ya SOMALIA na ETHIOPIA kukabidhi kwa hiari silaha wanazomiliki kinyume cha sheria.

 

Mpango huo wa kiusalama unatekelezwa katika hali ambayo hapo mwakani wananchi wa SOMALIA wanatarajiwa kushiriki katika zoezi la uchaguzi mkuu.

 

Aidha KENYA nayo mwakani inatarajiwa kuitisha uchaguzi ambapo Rais UHURU KENYATTA anatarajiwa kuwania uongozi kwa muhula wa pili.

 

KENYA imekuwa ikiandamwa na mashambulio ya wanamgambo wa AL-SHABAB kutokana na hatua yake ya kupeleka kikosi cha jeshi nchini SOMALIA chini ya mwavuli wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika kwa lengo la kupambana na wanamgambo hao.

 

 

GHANIA JUMBE

DESEMBA 5, 2016

 

 

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI