Madaktari KENYA wamekataa nyongeza zaidi iliyopendekezwa na Serikali
Madaktari nchini KENYA wamekataa nyongeza zaidi iliyopendekezwa hivi karibuni na serikali katika juhudi za kujaribu kumaliza mgomo wa madaktari na wahudumu wa afya ambao umedumu kwa mwezi mmoja sasa.
Madaktari wa KENYA wakimhudumia Mgonjwa katika moja ya Hospitali nchini humo. Madaktari hao wamekataa nyongeza zaidi ya malipo ilyopendekezwa na Serikali ya nchi hiyo hivi karibuni.

Madaktari nchini KENYA wamekataa nyongeza zaidi iliyopendekezwa hivi karibuni na serikali katika juhudi za kujaribu kumaliza mgomo wa madaktari na wahudumu wa afya ambao umedumu kwa mwezi mmoja sasa.

 

Mgomo huo umezorotesha huduma katika hospitali na zahanati za umma.

 

Rais UHURU KENYATTA amekutana na wawakilishi wa Chama cha Taifa cha Madaktari hao siku ya jumanne na kupendekeza nyongeza ya mshahara na marupurupu ya madaktari kwa angalau Dola za MAREKANI 560.

 

Mshahara huo ungesababisha madaktari wanaoanza kazi kulipwa takriban Dola Elfu MBILI kila mwezi.

 

Viongozi wa chama hicho wamesema pendekezo la serikali linawafaa madaktari lakini kuna baadhi ya mambo ya kuwafaa wananchi ambayo yameachwa nje.

 

Madaktari hao wanaitaka serikali kutekeleza makubaliano ya mishahara na marupurupu yaliyotiwa saini mwaka 2013.

 

Kwenye makubaliano hayo serikali iliahidi kuongeza idadi ya madaktari, kuongeza fedha za utafiti wa kimatibabu, dawa, vifaa na mitambo katika hospitali za umma.

 

 

GHANIA JUMBE

JANUARI 07,2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI