Jukwaa la Katiba DRC kusaini makubaliano
Jukwaa la katiba la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo –DRC limetangaza kuwa litatia saini makubaliano ya kisiasa yaliyofikiwa hivi karibuni.
Mratibu wa jukwaa la katiba la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo –DRC, Eve Bazaïba

 limetangaza kuwa litatia saini makubaliano ya kisiasa yaliyofikiwa hivi karibuni.

 

Mratibu wa jukwaa hilo, Eve Bazaïba amesema mjini Kinshasa kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya wasuluhishi kutambua madai yao ya kushika madaraka kwa mujibu wa katiba na si vinginevyo.

 

 Bazaïba amesema hatua hiyo ya kukubali kujumuika kwenye makubaliano hayo yaliyopitishwa tarehe 31 mwezi uliopita ni kutekeleza wito wa Umoja wa Mataifa wa kutaka pande zote zinazopingana katika jamhuri hiyo kushiriki kwenye mchakato huo kwa maslahi ya wananchi wote.

 

Kwa mujibu wa makubaliano hayo ya Disemba 31, Rais Joseph Kabila wa nchi hiyo amekubali kuachia madaraka mwishoni mwa mwaka huu .

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limetaka utekelezaji wa haraka wa mkataba huo ili kumaliza mgogoro wa kisiasa – DRC.

 

 

MARTHA NGWIRA

JANUARI 06, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI