Sudan Kusini kuendelea kupokea msaada kupitia Sudan
Serikali za Sudan na Sudan Kusini zimekubaliana kuongeza muda wa miezi sita ili Sudan Kusini iendelee kupokea msaada wa kibinadamu kupitia Sudan.
Balozi wa SUDAN Kusini nchini SUDAN, MAYAN DUT WAAL

Serikali za Sudan na Sudan Kusini zimekubaliana kuongeza muda wa miezi sita ili Sudan Kusini iendelee kupokea msaada wa kibinadamu kupitia Sudan .

 

Mapatano hayo yalitiwa saini Alhamis mjini Khartoum kati ya Naibu Kamishna wa ofisi ya msaada wa kibinadamu ya SUDAN,  AHMED MOHAMED OSMAN na balozi wa SUDAN Kusini MAYAN DUT WAAL

 

OSMAN amesema kuongezwa muda wa makubaliano hayo kunaweza kuimarisha uhusiano kati ya nchi mbili hizo ambapo pia amesisitiza kuwa serikali ya SUDAN iko tayari kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kufikisha msaada wa kibinadamu kwa wahitaji nchini Sudan Kusini

 

Makubaliano hayo yanaliwezesha Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa –WFP- nchini SUDAN kuwapatia msaada wa chakula watu zaidi ya laki mbili walioko mkoa wa Upper Nile huko SUDAN Kusini.

 

 

MARTHA NGWIRA

JANUARI 06, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI