Wakimbizi wa Somalia kuendelea kuhifadhiwa
Nchi tano za pembe ya Afrika zinazowahifadhi wakimbizi wa Somalia, zimesema zitaendelea kuwahifadhi wakimbizi hao wakati Jumuiya ya kimataifa ikiendelea na harakati za kurejesha amani ya kudumu nchini mwao.
Wakimbizi wa SOMALIA

Mjumbe maalum wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa – UNHCR-  Mohammed Abdi Affey amesema marais wa nchi za Ethiopia, Djibouti, Kenya, Somalia, Uganda na Yemen wamekubali kuendelea kuhifadhi wakimbizi hao.

Hata hivyo Affey amesema kuna haja ya kuongeza maradufu jitihada za kuleta amani nchini Somalia na usaidizi zaidi kwa wenyeji wanaohifadhi wakimbizi ili kupunguza msuguano kati ya wakimbizi na wenyeji.

MARTHA NGWIRA

JANUARI 06, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI