Kiwanda cha kuzalisha chakula cha kuku chazinduliwa
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia mifugo, Dkt. Mary Mashingo amezindua kiwanda kidogo cha kuzalisha chakula cha kuku cha kampuni ya PIL Trade Animal Feeds kilichopo Visiga mkoani Pwani.

Akizindua kiwanda hicho Dkt. Mashingo amewahakikishia wawekezaji wa vyakula vya mifugo kuwa serikali imeweka mazingira mazuri ya uanzishwaji wa viwanda ili wafugaji wawe na uhakika wa kupata malighafi.

Naye mmiliki wa kiwanda hicho Ismail ameiomba serikali kumsaidia kumalizia kiwanda hicho ambacho ameanza ujenzi ili aweze kuzalisha kati ya tani 300 hadi 600 za chakula cha kuku kwa siku.

VUMILIA MWASHA

JANUARI 06, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI