Rufani kupinga utozaji kodi zaongezeka mwaka 2016
Kesi za rufani kupinga utozaji wa kodi kati ya walipakodi na mamlaka ya mapato nchini -TRA zimeongezeka mara dufu mwaka jana 2016 hadi kufikia kesi 280 zilizoendeshwa na Bodi ya rufani za kodi.
Afisa sheria wa bodi ya rufani za kodi, Sekela Mwabukusi

Kesi za rufani kupinga utozaji wa kodi kati ya walipakodi na mamlaka ya mapato nchini -TRA zimeongezeka mara dufu mwaka jana 2016 hadi kufikia kesi 280 zilizoendeshwa na Bodi ya rufani za kodi.

Afisa sheria wa bodi ya rufani za kodi Sekela Mwabukusi amesema wamehukumu kesi 201 mwaka jana zenye ubishani wa shilingi bilioni 343 ambazo asilimia 50 ya kesi hizo mamlaka ya mapato TRA ilishinda.

Mwabukusi amesema awali walikuwa wakipokea kesi 50 kwa mwaka hivyo kuongezeka kwa kesi hizo kunatokana na uelewa wa walipakodi kiasi wanachotakiwa kulipa wanapopitisha mizigo bandarini au huduma wanazotoa.

STANLEY GANZEL

JANUARI 05, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI