Hisa za TOL zimepanda kwa asilimia tano na kuonoza kwa mwaka 2016
Hisa za Kampuni ya gas ya Tanzania -TOL- zimepanda kwa asilimia tano na hivyo kuwa miongoni mwa hisa za kampuni tano zilizoongoza kwa kupanda kwa bei katika soko la hisa la DAR ES SALAAM- DSE- mwaka uliopita wa 2016.
Soko la hisa la Dar es Salaam

Hisa za Kampuni ya gas ya Tanzania -TOL- zimepanda kwa asilimia tano na hivyo kuwa miongoni mwa hisa za kampuni tano zilizoongoza kwa  kupanda kwa bei katika soko la  hisa la DAR ES SALAAM- DSE- mwaka uliopita wa 2016.

Afisa mwandamizi wa DSE ,MARY KINABO amesema hisa za TOL ambazo zilianza kuuzwa kwenye soko hilo kwa bei ya shilingi 200 kwa hisa mwaka 1999, mwaka jana bei ya hisa hizo ilipanda kutoka shilingi 760 hadi shilingi 800.

KINABO amesema hisa nyingine ambazo zimeongoza kwa kupanda bei ni za benki ya NMB, kampuni madini ya ACACIA, kampuni ya usafirishaji KA, na kampuni ya bima ya JHL.

VUMILIA MWASHA

JANUARI 03, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI