Waziri wa Mazingira wa BURUNDI ameuwawa kwa kupigwa risasi
Waziri wa Mazingira wa BURUNDI ameuwawa kwa kupigwa risasi. Waziri EMMANUEL NIYONKURU alishambuliwa na mtu asiyejulikana wakati akielekea nyumbani.
Aliyekuwa waziri wa Mazingira wa BURUNDI, marehemu EMMANUEL NIYONKURU, aliyeuwawa kwa kupigwa risasi.

Waziri wa Mazingira wa BURUNDI ameuwawa kwa kupigwa risasi. Waziri EMMANUEL NIYONKURU alishambuliwa na mtu asiyejulikana wakati akielekea nyumbani.

Mauaji hayo yametokea kwenye maeneo ya ROHERO katika mji mkuu wa BUJUMBURA. Msemaji wa polisi PIERRE NKURIKIYE ameeleza kwamba wanamshikilia mwanamke mmoja kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.

Mauaji hayo ni ya kwanza kutokea yakimhusisha mtu mwenye wadhfa wa juu serikalini katika muda wa miaka miwili wa machafuko ya kisiasa yanayoendelea nchini BURUNDI.

JUDICA LOSAI

JANUARI 02, 2016

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI