Serikali ya KENYA yapiga marufuku wakazi wa MANDERA kutembea usiku
Serikali ya KENYA imeongeza muda wa kutotembea ovyo usiku kwa siku tisini kwenye mji wa MANDERA kufuatia mashambulio ya hivi karibuni yanayofanywa na wanamgambo wa al-Shabaab.
Waziri wa Mambo ya ndani wa KENYA, JOSEPH NKAISSERY

Serikali ya KENYA imeongeza muda wa kutotembea ovyo usiku kwa siku tisini kwenye mji wa MANDERA kufuatia mashambulio ya hivi karibuni yanayofanywa na wanamgambo wa  al-Shabaab. 

Waziri wa Mambo ya ndani wa KENYA, JOSEPH NKAISSERY amesema amri hiyo itatekelezwa hadi Machi 28 mwaka ujao na kuongeza kuwa itasaidia katika kudhibiti mashambulio yanayofanywa na wanamgambo.

Serikali ya KENYA ilitangaza amri ya kutotembea  kuanzia saa 12.30 jioni hadi 12.30 asubuhi kwa siku sitini kuanzia Oktoba 27 hadi Desemba 27 mwaka huu baada ya wanamgambo wa al shabaab kuwaua watu kumi na wawili katika hoteli moja nchini humo.

Hata hivyo NKAISSERY  amesema watu wanaweza kuruhusiwa kutembea kwa kibali kitakachotolewa na polisi kwenye maeneo yao.

MARTHA NGWILA

DESEMBA 30, 2016

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI