Taji la Miss World laenda Puerto Rico
Mrembo toka Puerto Rico, Stephanie Del Valle ametwaa taji la Miss World kwa mwaka 2016 baada ya kuwashinda warembo wengine toka kwenye nchi zaidi ya 100 kwenye shindano lilofanyika kwenye mji wa Maryland nchini, Marekani.
Mrembo kutoka Puerto Rico, Stephanie Del Valle ambaye ametwaa taji la Miss World kwa mwaka 2016.

Mrembo toka Puerto Rico, Stephanie Del Valle ametwaa taji la Miss World kwa mwaka 2016 baada ya kuwashinda warembo wengine toka kwenye nchi zaidi ya 100 kwenye shindano lilofanyika kwenye mji wa Maryland nchini, Marekani.

 

Mara baada ya kutawazwa kuwa mshindi mrembo huyo alisema ni heshima kwake na kwa nchi yake iliyoko kwenye visiwa vya Caribbean na amekuwa mrembo wa pili toka kwenye nchi hiyo kutwaa taji hilo la Miss world akitanguliwa na Wilnelia Merced alievishwa taji la Miss world mwaka 1975.

 

Mshindi wa pili kwenye shindano hilo la Miss World kwa mwaka huu ni Yaritza Miguelina Reyes Ramirez kutoka Jamhuri ya Dominica kutoka visiwa vya Caribbean na mshindi wa tatu anaitwa Natasha Mannuela kutoka Indonesia.

 

Mrembo toka Philippines, Catriona Elisa Gray pamoja na mrembo Evelyn Njambi kutoka Kenya ndio wanahitimisha orodha ya warembo walioingia kwenye nafasi ya tano bora ya Miss World kwa mwaka huu wa 2016.

 

Poto Rico inakuwa nchi ya 17 kutwa taji la Miss world mara mbili toka kuanzishwa kwa mashindano hayo mwaka 1951 huku nchi za Uingereza na India zikiongoza zikiwa zimetwaa taji hilo mara tano kila moja, Jamanica,Iceland zinafuata zikiwa zimetwaa taji hilo mara tatu.

 

 

MALYO CHETO

19 DESEMBA 2016

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI