Serikali kukuza mtaji wa TWIGA BANCORP
Ofisi ya msajili wa hazina imesema serikali imejipanga kukuza mtaji wa benki ya TWIGA BANCORP kwa kuisajili benki hiyo kwenye soko la hisa la DSM – DSE pamoja kupata wawekezaji wapya.
Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru akitoa ufafanuzi kuhusu jambo hilo mbele ya waandishi wa habari. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Twiga Bancorp, Cosmas Kimario

Akizungumzia mwenendo wa benki hiyo jijini DSM, Msajili wa hazina LAWRENCE MAFURU amesema mpango  huo utaiwezesha benki kutekeleza  miradi mbali kuongeza kiasi cha mikopo inayotolewa katika sekta ya uchumi.

 

Naye Afisa mtendaji mkuu wa benki hiyo COSMAS KIMARIO amemesema idadi ya mikopo iliyotolewa na benki hadi kufikia robo ya pili ya mwaka huu imeongezeka kwa asilimia 22.23 kutoka shilingi bilioni 38 hadi shilingi bilioni 47 mwaka huu.

 

July 18, 2016

FATUMA MATULANGA

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI