Waziri wa zamani wa ZIMBABWE aanzisha chama kipya cha siasa
Waziri wa zamani wa fedha wa ZIMBABWE, TENDAI BITI ameanzisha chama kipya cha kisiasa ikiwa ni matayarisho ya kumrithi rais ROBERT MUGABE
Waziri wa zamani wa fedha wa ZIMBABWE, TENDAI BITI

 Waziri wa zamani wa fedha wa ZIMBABWE, TENDAI BITI ameanzisha chama kipya cha kisiasa ikiwa ni matayarisho ya kumrithi rais ROBERT MUGABE wa nchini hiyo mwenye umri wa miaka TISINI na MOJA.

Chama hicho kipya Progressive Democratic Party – PDP  kimetangazwa ikiwa ni siku MBILI baada ya aliyekuwa makamu wa rais JOYCE MUJURU kutangaza azma ya kuunda chama chake.

Awali MUJURU alitajwa kuwa mrithi wa MUGABE kabla ya ugomvi wake na mke wa MUGABE, GRACE na hatimaye kufukuzwa serikalini. 

BITI naye alikuwa mwanachama wa chama kikuu cha upinzani  MDC lakini akaondoka baada ya chama hicho kushindwa uchaguzi kwa mara TATU mfululizo

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI