ICC yataka kuhamishia kesi nchini UGANDA
Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita – ICC imependekeza kesi dhidi ya mmoja wa viongozi wa kundi la waasi la UGANDA la Lord Resistace Army, DOMINIC ONGWEN ifanyike nchini UGANDA

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita – ICC imependekeza kesi dhidi ya mmoja wa viongozi wa kundi la waasi la UGANDA la  Lord Resistace Army, DOMINIC ONGWEN ifanyike nchini UGANDA huku mahakama hiyo ikifuta kesi dhidi ya kiongozi mwingine wa waasi hao.

Taarifa ya majaji wa mahakama ya ICC iliyotolewa hivi karibuni inasema haki inatekelezeka endapo kesi hiyo itafanyika karibu na eneo ilikofanyika uhalifu kwenye mji wa Kaskazini wa GULU au katika mji mkuu KAMPALA.

ONGWEN mwenye umri wa miaka AROBAINI aliingizwa kwenye uasi akiwa mtoto na baadaye akawa kiongozi wa LRA.

Mapema mwaka huu ONGWEN alishitakiwa kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.        

LRA chini ya uongozi wa JOSEPH KONI ililiuwa zaidi ya watu LAKI MOJA na kuwateka nyara watoto ELFU SITINI kufuiatia uasi ulioanza mwaka 1987 Kaskazini mwa UGANDA.

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI