Rais JAKAYA KIKWETE alihutubia bunge la KENYA
Rais JAKAYA KIKWETE amelihutubia bunge la KENYA na kusema serikali yake itahakikisha inalinda na kuimarisha ajenda ya utengamano ya AFRIKA MASHARIKI
Rais JAKAYA KIKWETE

Rais JAKAYA KIKWETE amelihutubia bunge la KENYA na kusema serikali yake itahakikisha inalinda na kuimarisha ajenda ya utengamano ya AFRIKA MASHARIKI.

 

Rais KIKWETE amesema nchi za AFRIKA MASHARIKI ni lazima ziungane ili ziweze kumudu ushindani katika soko la dunia hivyo kuimarisha hali ya uchumi miongoni mwa nchi wanachama.

 

Rais KIKWETE pia amewahakikishia wakenya kuwa TANZANIA itaendelea kushirikiana na KENYA hata baada ya yeye kumaliza muda wake na rais mwingine kuingia madarakani.

 

Amewaambia wabunge hao wa KENYA kuwa anafurahi kuondoka madarakani huku akiacha uhusiano mzuri kati ya TANZANIA na KENYA.

 

Rais JAKAYA KIKWETE amerejea nchini Jumanne jioni baada ya kukamilisha ziara ya siku TATU nchini KENYA.

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI