Fainali BONGO STAR SEARCH kufanyika ijumaa wiki hii
Fainali za Shindano la kuibua vipaji vya muziki la BONGO STAR SEARCH msimu wa nane linatarajia kufanyika siku ya ijumaa wiki hii katika ukumbi wa KING SOLOMON jijini DSM
RITA PAULSEN

Fainali za Shindano la kuibua  vipaji vya muziki la BONGO STAR SEARCH msimu wa nane  linatarajia kufanyika siku ya ijumaa wiki hii katika ukumbi wa KING SOLOMON jijini DSM.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini DAR ES SALAAM Jaji mkuu wa Shindano hilo  RITA PAULSEN amesema washiriki SITA wameingia katika fainali hizo ikiwa ni matokeo ya mchujo kutoka kwa washiriki 20 waliofanikiwa kuingia katika kambi ya mwisho ya mashindano hayo.

SAMSON MAJALIWA kutoka  kampuni ya simu ya HUWAEI ambao wanadhamini shindano hilo wameahidi zawadi za simu kwa washindi.

Mshindi wa shindano hilo atapata shilingi  MILIONI 60.

Kiingilio katika shindano hilo kitakua shilingi ELFU 25 kwa viti vya kawaida, VIP shilingi ELFU 50 na viti vya VIP maalum itakua shilingi LAKI MOJA.

Shindano hilo litasindikizwa na wanamuziki mbalimbali wa hapa nchini na GALLARDO kutoka NIGERIA

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI