VPL kutimua vumbi 12 septemba
Msimu mpya wa ligi kuu TANZANIA bara unaanza tarehe 12 septemba kwa viwanja saba na timu kumi na nne kushuka dimbani kusaka pointi kwenye michezo yao ya kwanza
VPL kutimua vumbi 12 sept

 Msimu mpya wa ligi kuu TANZANIA bara unaanza tarehe 12 septemba kwa viwanja saba na timu kumi na nne kushuka dimbani kusaka pointi kwenye michezo yao ya kwanza.

Ligi hiyo ya mwaka huu inajumuhisha timu kumi na sita tofauti na msimu uliopita uliokuwa na timu kumi na nne ambapo kuna ongezeko la timu mbili.

Timu mpya ambazo zimepanda daraja msimu huu ni NNE ambazo ni MWADUI FC ya SHINYANGA,TOTO AFRICA ya MWANZA, MAJIMAJI ya SONGEA na AFRICAN SPORTS ya TANGA na zote hizo zitashuka dimbani siku ya kwanza kabisa ya ufunguzi wa ligi hiyo.

Moja ya michezo ya kuvutia siku hiyo ya kwanza ya ligi kuu ni baina ya AFRICAN SPORTS dhidi ya SIMBA utaochezwa kwenye uwanja wa MKWAKWANI , AZAM FC dhidi ya TANZANIA PRISONS itakayochezwa kwenye uwanja wa AZAM COMPLEX na MBEYA CITY watakaocheza na KAGERA SUGAR kwenye uwanja wa SOKOINE mjini MBEYA.

Mabingwa wa tetezi wa ligi hiyo timu ya YANGA wenyewe watashuka dimbani siku ya jumapili kucheza na COASTAL UNION ya TANGA kwenye dimba la TAIFA hapa jijini DAR ES SALAAM.

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI