Basi la Smart lanusurika kusombwa maji
Basi moja la abiria la kampuni ya SMART, lililokuwa likitokea nchini Kenya, kwenda Tanzania, limenusurika kusombwa na maji baada ya mafuriko kuikumba nchi hiyo

Basi moja la abiria la kampuni ya SMART, lililokuwa likitokea nchini Kenya, kwenda Tanzania, limenusurika kusombwa na maji baada ya mafuriko kuikumba nchi hiyo na kusababisha barabara kuu Muhoroni-Londiani kujaa maji.

 

Basi hilo lilisababisha shughuli za usafiri kusimama katika kivuko cha Lekoni, ambako lilikwama lilipokuwa likijaribu kuvuka kwenda upande wa pili.

 

Hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa kutokana na msukosuko huo wa mafuriko nchini Kenya.

 

Nyambona Massamba

12 May 2016

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI