STURRIDGE arejea dimbani
Mshambuliaji wa LIVERPOOL, Daniel Sturridge amerejea dimbani na kuanza mazoezi na timu hiyo toka kufanyiwa upasuaji wa misuri ya nyama za paja mwezi MAY mwaka huu
Mshambuliaji wa LIVERPOOL, Daniel Sturridge

Mshambuliaji wa LIVERPOOL, Daniel Sturridge amerejea dimbani na kuanza mazoezi na timu hiyo toka kufanyiwa upasuaji wa misuri ya nyama za paja mwezi MAY mwaka huu.

Mshambuliaji huyo hajacheza mchezo wowote toka alipoichezea LIVERPOOL kwa mara ya mwisho kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya BLACKBURN ROVERS na alitumia kipindi chote cha msimu wa kiangazi kupata matibabu nchini MAREKANI.

Taarifa zinasema pamoja na kurejea dimbani Sturridge hawezi kucheza mchezo wa kesho wa ligi kuu ya ENGLAND dhidi ya Manchester United.

Msimu uliopita mshambuliaji huyo aliichezea LIVERPOOL michezo 18 na kufunga magoli matano ila kabla ya hapo msimu mmoja nyuma alifunga magoli 24 kwenye michezo 33 na kuisaidia LIVERPOOL kushika nafasi ya pili kwenye ligi kuu ya ENGLAND.

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI