Watumishi wasio waaminifu kufukuzwa kazi KENYA
Uongozi wa serikali ya KENYA katika kaunti ya KARAKANIDHI, umetishia kuwafukuza kazi wafanyakazi wa hospitali ya serikali ya CHUKA wanaotuhumiwa kuiba mashine moja ya kupimia magonjwa mbalimbali hospitalini hapo

Mashine hiyo mali ya serikali ina thamani ya zaidi ya shilingi Milioni tatu za KENYA. Serikali kuu nchini KENYA hivi karibuni, ilitoa mashine hiyo kwa hospitali ya CHUKA ili kuboresha huduma za afya katika eneo hilo.

Serikali ya KENYA, imeamua kuingilia kati tukio hilo, kwani hivi karibuni, ulitokea wizi wa pikipiki za serikali, zilizokuwa zikitumika kutoa huduma mbalimbali katika hospitali ya CHUKA.

 

May 4, 2016

NYAMBONA MASABA

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI