BOKO HARAM yatoa picha ya baadhi ya wanafunzi waliotekwa
Kikundi cha wanamgambo wa kiislam cha BOKO HARAM nchini NIGERIA kimetoa picha ya video inayoonyesha baadhi ya wanafunzi wa kike waliotekwa miaka miwili iliyopita katika mji wa CHIBOK
BOKO HARAM yatoa picha ya baadhi ya wanafunzi waliotekwa

Habari zinasema picha hizo ambazo zimerekodiwa mwezi Disemba zimewasilishwa katika serikali ya NIGERIA zikionyesha wasichana 15 waliovalia mavazi na kujitambulisha kuwa miongoni mwa wanafunzi waliotekwa wakiwa shule.

 

Baadhi ya wazazi wa watoto hao wamekiri kuwatambua.

 

Hii ni mara ya kwanza kuonyeshwa kwa picha za wanafunzi hao tangu mwezi Mei mwaka 2014 ambapo wasichana 276 walitekwa.

 

April 14, 2016

NYAMBONA MASAMBA

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI