Wachezaji 24 wa Taifa stars waitwa kuikabili Malawi
Jumla ya wachezaji ishirini na nne wameitwa kuunda kikosi cha timu ya TAIFA ya soka ya TANZANIA, TAIFA STARS kujiandaa na mchezo wa kufuzu
Wachezaji 24 wa Taifa stars waitwa kuikabili Malawi

Jumla ya wachezaji ishirini na nne wameitwa kuunda kikosi cha timu ya TAIFA ya soka ya TANZANIA, TAIFA STARS kujiandaa  na mchezo wa kufuzu kwa kombe la dunia dhidi ya MALAWI,mchezo utakaochezwa OCTOBA SABA jijini DSM.

Kocha msaidizi wa TAIFA STARS, HEMED MOROCCO amesema mchezo huo ni muhimu mno kwao na wamepanga kuumaliza mapema kwa kupata ushindi mnono kwenye mchezo wa kwanza.

MOROCCO amesema wameita wachezaji wale wale waliocheza dhidi ya NIGERIA kutokana na muda wa maandalizi kuwa mfupi na kusisitiza,STARS itacheza mchezo wa kushambulia zaidi dhidi ya MALAWI ili kuibuka na ushindi wa mabao mengi.

Kikosi hicho kitakuwa na wachezaji wanne wa kimataifa ambao ni Mbwana Samatta na Thomasi Ulimwengu wa TP Mazembe na Mrisho Ngassa wa Free state Stars ya Africa Kusini.

Mchezo huo wa kwanza wa kufuzu kwa kombe la DUNIA dhidi ya MALAWI utachezwa hapa nchini kwenye dimba la TAIFA, OCTOBER SABA na kurudiana nchini MALAWI siku nne baadae.

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI