BASHIR aahidi mwaka 2016 kuwa wa amani nchini SUDAN
Rais OMAR AL BASHIR wa SUDAN amesema suala la harakati za waasi nchini humo litakuwa limehitimishwa kikamilifu ifikapo mwaka ujao wa 2016
Rais OMAR AL BASHIR wa SUDAN

Rais OMAR AL BASHIR wa SUDAN amesema suala la harakati za waasi nchini humo litakuwa limehitimishwa kikamilifu ifikapo mwaka ujao wa 2016.

Rais BASHIR ametoa ahadi hiyo katika hafla ya kumtambulisha Waziri mpya wa Ulinzi na kusisitiza kwamba mwaka ujao utakuwa mwaka wa amani nchini Sudan, na harakati za makundi ya waasi nchini humo zitahitimishwa kikamilifu.

 

Wakati huo huo Waziri mpya wa Ulinzi wa SUDAN AWADH MUHAMMAD AHMAD IBN AUF ametoa wito kwa makundi ya waasi na ya wabeba silaha kujiunga na mazungumzo ya kitaifa.

 

Amesema milango ya kutafuta suluhu ingali iko wazi na bado kuna fursa ya kujiunga na mchakato wa amani.

 

Vikosi vya Jeshi la SUDAN vinapambana na makundi ya waasi wanaobeba silaha katika maeneo ya DARFUR Magharibi pamoja na BLUE NILE na KORDOFAN KUSINI huko Kusini mwa nchi hiyo.

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI