Mgombea wa Urais Marekani TRUMP anusurika kupigwa
Mgombea wa kiti cha urais nchini MAREKANI kupitia Chama cha REPUBLICAN, DONALD TRUMP amenusurika kupigwa kutokana na maneno yake makali ya chuki
Mgombea wa kiti cha urais nchini MAREKANI kupitia Chama cha REPUBLICAN, DONALD TRUMP

Mgombea wa kiti cha urais nchini MAREKANI kupitia Chama cha REPUBLICAN, DONALD TRUMP amenusurika kupigwa kutokana na maneno yake makali ya chuki ambayo mara kadhaa yamezua hasira miongoni mwa watu.

Walinzi waliokuwa wakidhibiti usalama katika kampeni za TRUMP Mjini OHIO walilazimika kumtia mbaroni mtu mmoja aliyeamua kuvunja safu wa walinzi wa TRUMP na kwenda moja kwa moja kumvamia kiongozi huyo.

Wanasiasa kadhaa nchini MAREKANI wakiwemo wagombea wa kiti cha urais wameshutumu vikali kauli za TRUMP kwenye kampeni zake ambazo mara kadhaa zimezidi kuchochea masuala ya ubaguzi na itikadi za watu.

Mgombea kiti cha urais nchini humo kupitia Chama cha REPUBLICAN aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa MAREKANI, HILLARY CLINTON amesema wanasiasa wanapaswa kuwaunganisha wananchi wa MAREKANI, badala ya kutoa kauli za kuwagawanya.

 MARCH 13,2016
GHANIA JUMBE

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI