Rais MAGUFULI ateua wakuu wa Mikoa 26
Rais JOHN MAGUFULI amefanya uteuzi wa wakuu wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara ambapo kati yao 13 ni wapya, SABA wamebakizwa katika vituo vyao vya kazi
Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi ambaye pia ni Katibu Mkuu TAMISEMI, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe akitangaza Majina ya Wakuu wapya wa Mikoa kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam

Rais JOHN MAGUFULI amefanya uteuzi wa wakuu wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara ambapo kati yao 13 ni wapya, SABA wamebakizwa katika vituo vyao vya kazi, WATANO wamehamishwa vituo vya kazi na MMOJA amepangiwa Mkoa Mpya wa SONGWE.

Uteuzi huo umetangazwa na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi MUSSA IYOMBE Ikulu Jijini DSM.

Walioteuliwa kushika wadhufa huo wa Ukuu wa Mkoa ni PAUL MAKONDA ambaye anakua Mkuu wa Mkoa wa DSM, Meja Jenerali Mstaafu EZEKIEL KYUNGAMkuu wa Mkoa wa GEITA,Meja Jenerali Mstaafu SALUM KIJUU Mkuu wa Mkoa wa KAGERA, Meja Jenerali Mstaafu RAPHAEL MUHUGA Mkuu wa Mkoa wa KATAVI na Brigedia Jeneral Mstaafu EMMANUEL MAGANGA amteteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa KIGOMA.

Wengine ni GODFREY ZAMBI ambaye anakuaMkuu wa Mkoa wa LINDI,Dokta STEVEN KEBWE Mkuu wa Mkoa wa MOROGORO,Kamishna Mstaafu wa Polisi ZELLOTHE STEVEN Mkuu wa Mkoa wa RUKWA, ANNA MALECELA KILANGO  Mkuu wa Mkoa wa SHINYANGA naMhandisi METHEW MTIGUMWE ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa SINGIDA.

ANTONY MATAKA ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa SIMIYU, AGGREY MWANRI Mkuu wa Mkoa wa TABORA, MARTINE SHIGELAMkuu wa Mkoa wa TANGA,JORDAN RUGIMBANA - Mkuu wa Mkoa DODOMA,SAID MECK SADICK Mkuu wa Mkoa KILIMANJARO,MAGESA MULONGO, Mkuu wa Mkoa MARA, AMOS MAKALLA - Mkuu wa Mkoa MBEYA, JOHN MONGELLAanakua Mkuu wa Mkoa MWANZA, FELIX NTIBENDAMkuu wa Mkoa wa ARUSHA na AMINA MASENZA Mkuu wa Mkoa wa IRINGA.

Wengine ni JOEL BENDERA Mkuu wa Mkoa wa MANYARA, HALIMA DENDEGU Mkuu wa Mkoa wa MTWARA, Dokta REHEMA NCHIMBI Mkuu wa Mkoa wa NJOMBE, Mhandisi EVARIST NDIKILO Mkuu wa Mkoa wa PWANI, SAID MWAMBUNGU Mkuu wa Mkoa RUVUMA na Luteni Mstaafu CHIKU GALAWAMkuu wa Mkoa Mpya wa SONGWE.

Wakuu wote wa mikoa walioteuliwa wataapishwa Jumanne tarehe 15 mwezi huu Saa 3:30 Asubuhi Ikulu Jijini DSM.

 MARCH 13,2016
TAARIFA IKULU

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI