Uwezo wa wafanyabisahara wa ndani kupata mikopo mikubwa waongezeka
Wafanyabiashara nchini wanauwezo wa kupata mikopo ya hadi dola milioni 500 za Marekani katika benki ya Maendeleo ya Biashara Afrika –AFREXIMBANK
benki ya Maendeleo ya Biashara Afrika –AFREXIMBANK

Wafanyabiashara nchini wanauwezo wa  kupata mikopo ya hadi dola milioni 500 za Marekani katika  benki ya Maendeleo ya Biashara Afrika –AFREXIMBANK- kwa sababu Tanzania ni miongoni mwa wamiliki wa benki hiyo.                                                                                                                        

Akizungumza na wafanyabiashara wa Tanzania jijini DSM, Mkurugenzi wa maendeleo ya miradi wa benki hiyo JOHN KOFI amesema mikopo hiyo ni ya muda mfupi na ni kwa ajili ya wafanyabiashara waliowekeza kwenye sekta za viwanda, biashara, madini na hoteli.

 

 Naye naibu gavana wa benki kuu LILA MKILA amesema serikali imewekeza fedha nyingi kwenye benki hiyo ili kuruhusu wafanyabiashara, zikiwemo taasisi za fedha kupata mitaji kwa urahisi.

 

Wakati huo huo idadi ya  hoteli  za kitalii zinazomilikiwa kwa asilimia mia moja na watanzania inaongezeka baada ya mitaji kuanza kupatikana kwa urahisi.

 

Meneja masoko wa hoteli  ya kitalii ya Mbezi Garden ya jijini DSM RICHARD MOSHA amesema hoteli nyingi za kitalii nchini zimejengwa na watanzania kutokana na upatikanaji kwa urahisi wa mitaji.

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI