Mpango wa nyuklia wa IRAN moja ya mada kuu za wagombea urais MAREKANI
Mpango wa nyuklia wa IRAN, imekuwa ni moja kati ya mada kuu miongoni mwa wagombea wa kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa MAREKANI
HILARRY CLINTON

Mpango wa nyuklia wa IRAN, imekuwa ni moja kati ya mada kuu miongoni mwa wagombea wa kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa MAREKANI.

Wagombea mbalimbali wanaelezea jinsi watakavyochukua hatua mbalimbali za maamuzi kuhusiana na mpango wa nyuklia wa IRAN. Miongoni mwa wagombea hao ni aliyekuwa waziri wa Mambo ya nje wa MAREKANI, HILARRY CLINTON.

Amesema nchi yake itafuatilia kwa karibu mpango huo wa nyuklia wa IRAN, kuhakikisha kuwa hauleti athari kwa jumuiya ya kimataifa, pamoja na nchi ya MAREKANI.

CLINTON amesema akichaguliwa kuiongoza nchi hiyo hata sita kuchukua hatua kali dhidi ya IRAN, ikiwemo ya kijeshi kuidhibiti IRAN endapo mpango wake huo utahatarisha usalama.

IRAN imekuwa ikipata shinikizo la kimataifa kuhusiana na mpango wake wa nyuklia, ambapo imekuwa ikionekana kama inataka kutengeneza silaha za maangamizi. Hata hivyo nchi hiyo imekuwa ikisisitiza kuwa mpango wake huo wa nyuklia ni wa amani

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI