KENYATTA awagomea walimu nchini KENYA
Wakati shule zote za umma na binafsi zikianza kufungwa kuanzia hii leo nchini KENYA, Rais wa nchi hiyo UHURU KENYATTA amelihutubia taifa kwa njia ya televisheni
Rais UHURU KENYATTA wa KENYA

Wakati shule zote za umma na binafsi zikianza kufungwa kuanzia hii leo nchini KENYA, Rais wa nchi hiyo UHURU KENYATTA amelihutubia taifa kwa njia ya televisheni na kusema kuwa serikali ya nchi hiyo haina uwezo wa kulipa nyongeza ya mishahara wanayodai walimu wanaoendelea na mgomo.

 

Rais KENYATTA ametoa wito mgogoro huo kutatuliwa kwa amani na kusema kuwa shule zote zinafungwa kuanzia leo.

 

Serikali ya KENYA imeagiza shule zote nchini humo zifungwe kuanzia leo huku mgomo wa walimu ukiendelea.

 

Barua kutoka kwa Wizara ya Elimu imeagiza shule zote za umma na za kibinafsi zifungwe na wanafunzi warudi nyumbani.

 

Watakaobaki shuleni ni wanafunzi wanaojiandaa kufanya mitihani ya kitaifa ya Darasa la NANE na Kidato cha NNE mwaka huu.

 

Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu nchini KENYA -KNUT amesema tayari amepokea barua hiyo ya kufungwa kwa shule kutoka kwa serikali.

 

Siku ya Ijumaa mahakama inatarajiwa kuamua iwapo mgomo huo wa walimu ambao umelemaza masomo muhula wa tatu ni halali ama la.

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI