Mauzo soko la hisa yaongezeka
Mauzo ya soko la hisa la DSM - DSE yameongezeka kwa zaidi ya shilingi bilioni mia sita mwaka uliopita wa 2015 baada ya watanzania wengi kujitokea kuwekeza fedha zao kupitia soko hilo
Meneja wa fedha na utafiti wa DSE, IBRAHIM MSHINDO

Mauzo ya soko la hisa la DSM - DSE  yameongezeka kwa zaidi ya shilingi bilioni mia sita mwaka uliopita wa 2015 baada ya watanzania wengi kujitokea kuwekeza fedha zao kupitia soko hilo.

 

Akitoa tathmini ya mwenendo wa soko kwa mwaka uliopita, meneja wa fedha na utafiti wa DSE, IBRAHIM MSHINDO amesema mauzo yameongezeka kutoka shilingi bilioni 383 mwaka 2014 hadi shilingi tirioni 1.1 mwaka 2015.

 

Amesema idadi ya kampuni zilizosajiliwa kwenye soko hilo pia ziliongezeka kutoka kampuni 21 hadi kampuni 22 na idadi ya wawekezaji wa ndani iliongezeka kwa asilimia 2.1 ambapo hisa za kampuni ya TOL, CRDB, DCB, TBL, TCC zilifanya vizuri mwaka jana.

 

Tarehe 04 january 2016

Na  FATUMA MATULANGA

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI