Kukithiri kwa uchafu mkoani MWANZA kikwazo cha kupambana na kipindupindu
Halmashauri ya jiji la MWANZA inakabiliwa na changamoto ya kudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu kutokana na kukithiri kwa uchafu katika baadhi ya maeneo ya jiji hilo

Halmashauri ya jiji  la MWANZA inakabiliwa na changamoto ya  kudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu kutokana na kukithiri kwa uchafu katika baadhi ya maeneo ya jiji hilo.

 

Halmashauri ya jiji la MWANZA ililazimika  kuchukua hatua za kudhibiti uuzaji holela wa vyakula, matunda na pombe za kienyeji, ili kuudhibiti ugonjwa huo.

 

Baadhi ya mama na baba lishe  ambao biashara zao zimefungwa wamesema kuwa zoezi hilo limefanyika kwa upendeleo kutokana na kuendelea kwa biashara za mama lishe katika baadhi ya maeneo ikiwemo soko kuu la MWANZA ambalo limezungukwa na uchafu.

 

Wakazi 928 wameugua  ugonjwa wa kipindupindu mkoani mwanza tangu septemba mwaka huu ambapo 25 kati yao wamepoteza maisha  kutokana na ugonjwa huo.

 

Tarehe 30 December 2015

Na AMICUS BUTUNGA

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI