Canavaro achoshwa na migogoro ya soka Zanzibar
NAHODHA wa timu ya taifa TANZANIA TAIFA STARS na timu ya YANGA NADIR HAROUB CANNAVARO ameonyesha kusikitishwa kwake jinsi hali ilivyo hivi sasa
NADIR HAROUB CANNAVARO

NAHODHA wa timu ya taifa TANZANIA TAIFA STARS na timu ya YANGA  NADIR  HAROUB CANNAVARO ameonyesha kusikitishwa kwake jinsi hali ilivyo hivi sasa kwenye soka la nyumbani kwao ZANZIBAR.

CANAVARO ameimbia TBC kuwa migogoro iliyopo hivi sasa kwenye chama cha soka kisiwani humo ZFA ni pigo kubwa kwa muskatabali wa soka la kisiwani humo na kusema migogoro hiyo inarudisha nyuma maendeleo ya soka.

Pamoja na migogoro hiyo bado kuna wachezaji wengi toka kisiwani humo wanafanya vizuri kwenye ligi kuu TANZANIA BARA na wanaheshimiwa mno kutokana na uwezo wao wanaonyesha wakiwa dimbani.

Mmoja wa wachezaji ni mlinzi mpya wa timu ya Yanga, Haji Mwinyi ambae hivi sasa amekuwa ni kivutio kikubwa cha wapenda soka na moja kwa moja ameingia kwenye kikosi cha kwanza cha Taifa Stars.

Kutokana na migogo hiyo ligi kuu ya ZANZIBAR bado haijaanza kwasababu kunazuio mahakamani kitu ambacho kinakwamisha maendeleo ya soka.

Hivi karibuni shirikisho la soka barani Africa CAF kilifuta mafunzo ya ukocha ya lesini B yaliyotakiwa kufanyika kisiwani humo kutokana na mvutano huo wa uongozi ndani ya ZFA na kuwanyima makocha wengi wazawa kupanda kiwango cha ufundishaji wa soka.

Na Canavaro anawalilia wadau kuacha migongano hiyo kwamaana soka la sasa linaendeshwa kisasa na kuvutana kwao kutasababisha kushuka kiwango cha soka

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI