Babati yashindwa kukusanya mapato
Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Babati mkoani Manyara Fortunatus Fwema amesema halmashauri hiyo imeshindwa kukusanya mapato katika vyanzo vyake kwa kuwa wadau wake wa maendeleo hawana utamaduni wa kulipa kodi kwa hiari.

Fwema amesema katika mwaka wa fedha 2016/2017 halmashauri hiyo ililenga kukusanya zaidi ya shilingi Bilioni Sita lakini hadi kufikia Novemba 30 mwaka jana ilikuwa imekusanya shilingi Milioni 458.2 tu sawa na asilimia 7.49.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Mohamed Kibiki amewaomba wafanyabiashara wa mji wa Babati kulipa ushuru na kodi za serikali ili kuiwezesha Halmashauri kutekeleza majukumu yake.

NICO MWAIBALE

JANUARI 06, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI