Tozo za ushuru zapanda soko la samaki feri
Meneja Mkuu wa soko la kimataifa la samaki la feri jijini Dar Es Salaam, Mniko Eliakim amesema tozo mbalimbali za ushuru katika soko hilo zimepanda kuanzia mwezi huu ili soko hilo liweze kukusanya mapato ya kutosheleza kujiendesha.
Biashara ya Samaki sokono, Ferry

Meneja Mkuu wa soko la kimataifa la samaki la feri jijini Dar Es Salaam, Mniko Eliakim amesema tozo mbalimbali za ushuru katika soko hilo zimepanda kuanzia  mwezi huu ili soko hilo liweze kukusanya mapato ya kutosheleza kujiendesha.

Mniko amesema tozo zilizopanda ni pamoja na kodi ya kutwa kutoka shilingi 200 mpaka shilingi 1000 kwa siku, vizimba kutoka shilingi 6000 mpaka shilingi 10000 kwa mwezi, na waliopanga sehemu za kuhifadhi samaki kutoka shilingi 50000 kwa mwezi mpaka shilingi elfu 80000.

VUMILIA MWASHA

JANUARI 06, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI