CCM yazindua kampeni za uchaguzi mdogo Morogoro
Chama Cha Mapinduzi - CCM wilaya ya Morogoro Mjini kimezindua kampeni za uchaguzi mdogo katika kata ya Kiwanja Cha Ndege Manispaa ya Morogoro.

Chama Cha Mapinduzi - CCM wilaya ya Morogoro Mjini kimezindua kampeni za uchaguzi mdogo katika kata ya Kiwanja Cha Ndege Manispaa ya Morogoro.

Katika kampeni hiyo viongozi wa chama hicho wamemnadi mgombea Isihaka Sengo kwa wananchi wa kata hiyo kuwa wakimchagua watakuwa wamekichagua chama ambacho hadi sasa kimeonyesha mabadiliko makubwa ya huduma mbalimbali za kijamii.

Uchaguzi huo ambao utafanyika Januari 22 mwaka huu unafanyika kujaza nafasi iliyoachwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo God Mkondya ambaye amefariki mwanzoni mwa mwaka jana.

Vyama vinavyoshiriki katika uchaguzi huo mdogo ni CCM, CUF na CHADEMA.

MONICA LYAMPAWE

JANUARI 06, 2016

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI