Watu 14 wamekufa katika ajali Uganda
Watu 14 wamekufa na wengine tisa kujeruhiwa vibaya wakati gari la abiria lilipokuwa likijaribu kumkwepa ng’ombe na kisha kugongana na magari makubwa mawili eneo la Lwengo nchini Uganda.
Eneo la ajali, Mara baada ya ajali hiyo.

Watu 14 wamekufa na wengine tisa kujeruhiwa vibaya wakati gari la abiria lilipokuwa likijaribu kumkwepa ng’ombe na kisha kugongana na magari makubwa mawili eneo la Lwengo nchini Uganda.

Mkuu wa Polisi wa Kikosi cha Usalama barabarani wa Uganga, Scovia Birungi amesema watu wanane walikufa papo hapo akiwemo mwandishi wa habari na wengine sita walikufa baada ya kufikishwa hospitali.

Birungi amesema ajali hiyo imesababishwa na mwendo kasi wa gari la abiria lililokuwa likimkwepa ng’ombe  aliyekuwa akivuka barabara ambaye pia alikufa katika ajali hiyo.

MARTHA NGWIRA

JANUARI 05, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI