Mfumko wa bei waongezeka Zanzibar
Kasi ya mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwezi mmoja VISIWANI ZANZIBAR imeongezeka kwa asilimia 0.7 kutoka asilimia 2.3 mwezi Novemba hadi asilimia 3. 0 mwezi Disemba mwaka jana.
Mkuu wa kitengo cha takwimu za bei, wa ofisi ya mtakwimu mkuu wa serikali Zanzibar, KHAMIS AHMADA SHAURI

Kasi ya mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwezi mmoja VISIWANI ZANZIBAR imeongezeka kwa asilimia 0.7 kutoka  asilimia 2.3 mwezi Novemba hadi asilimia  3. 0 mwezi Disemba mwaka jana.

Akitoa taarifa ya mfumuko wa bei mjini UNGUJA,  Mkuu wa kitengo cha takwimu za bei, wa ofisi ya mtakwimu mkuu wa serikali Zanzibar,  KHAMIS AHMADA SHAURI amesema ongezeko hilo pia limechangiwa na kuongezeka kwa bei ya bidhaa za vyakula, na vinywaji visivyo na kilevi kwa asilimia 1.2 mwezi  Disemba kutoka asilimia 0.4 mwezi Novemba nwaka 2016.

Pia amesema kupanda kwa bei ya nishati za mafuta na mkaa kumechangia kuongezeka kwa kasi mfumuko wa bei kwa mwezi Disemba.

STANLEY GANZEL

JANUARI 05, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI