Serikali yashauriwa kuwafundisha walimu ukocha
SERIKALI imeshauriwa kuweka mipango maalum ya kuwafundisha walimu wa shule za msingi taaluma ya ukocha wa soka ili watumie ujuzi huo kuibua na kuendeleza vipaji kwa wanafunzi wao.

SERIKALI imeshauriwa kuweka mipango maalum ya kuwafundisha walimu wa shule za msingi taaluma ya ukocha wa soka ili watumie ujuzi huo kuibua na kuendeleza vipaji kwa wanafunzi wao.

Rai hiyo imetolewa na katibu mkuu wa chama cha makocha nchini (TAFCA), MICHAEL  BUNDALA ambae amesema shule za msingi zinawanafunzi wengi na zinaweza kuwa chimbuko vizuri la mchezo wa soka.

Kwa upande wao wanafunzi wanaopata mafunzo hayo ya awali ya ukocha, FUNUA ALLY FUNUA na MRISHO HAMIS  wamesema mafunzo hayo yatasaidia kuboresha ufundishaji wao wa soka.

Jumla ya makocha 20 kutoka katika wilaya ya kinondoni hapa jijini DSM wanashiriki katika mafunzo hayo ya awali ya ukocha wa soka.

EVANCE MHANDO

DESEMBA13, 2016

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI