Wami – Mbiki hatarini kuvunjika
Jumuiya ya Hifadhi ya WAMI–MBIKI inayoshirikisha vijiji 24 vya wilaya za Morogoro, Bagamoyo na Mvomero iko hatarini kuvunjika.

Jumuiya ya Hifadhi ya WAMI–MBIKI inayoshirikisha vijiji 24 vya wilaya za Morogoro, Bagamoyo na Mvomero iko hatarini kuvunjika baada ya kushindwa kuwalipa askari wake mishahara ya zaidi ya miaka minne inayofikia zaidi ya shilingi milioni 60.

 

Wawakilishi wa jumuiya hiyo wamedai kuwa wawekezaji wa hifadhi hiyo wamejitoa baada ya hifadhi kuvamiwa na mifugo,ujangili wa wanyama na magogo huku wakimtuhumu Mwenyekiti wao Majuka Koira kuwa chanzo cha kuanguka kwa Jumuiya yao.

 

Jumuiya ya Wami-Mbiki inalelewa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

 

 

PRAXEDA MTANI

NOVEMBA 17, 2016

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI