Mazungumzo ya Amani MSUMBIJI yaanza upya
Mazungumzo ya amani kati ya serikali ya MSUMBIJI na chama kikuu cha upinzani nchini humo cha Renamo yameanza tena wiki moja baada ya kusitishwa kufuatia mauaji ya mzungumzaji mkuu wa upande upinzani.

Msuluhishi wa kimataifa katika mazungumzo hayo MARIO RAFFAELLI  ametangaza kuanza tena kwa mazungumzo hayo baada ya kukutana na pande mbili zinazohusika katika mazungumzo ya kuleta amani nchini MSUMBIJI.

Mzungumzaji huyo wa upande wa upinzani  JEREMIAS PONDECA ambaye pia ni mjumbe wa tume ya pamoja iliyoundwa kutafuta njia zitakazoweza kumaliza tofauti kati aya serikali ya MSUMBIJI na Renamo aliuawa Oktoba saba mwaka huu wakati akifanya mazoezi katika mji mkuu wa nchi hiyo MAPUTO.

Oktoba 19, 2016

MARTHA NGWIRA

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI