Rais wa Afrika ya Kati asema ongezeko la ghasia linatishia mustakabali wa nchi
Rais FAUSTIN-ARCHANGE TOUADERA wa Jamhuri ya AFRIKA ya Kati amesema kuongezeka kwa ghasia na matumizi ya nguvu nchini humo ni tishio kwa mustakabali wa nchi hiyo

Rais TOUADERA amesema mapigano yaliyozuka  hivi karibuni katika mji mkuu wa nchi hiyo BANGUI na  mji mkuu na miji mingine mitatu yanahatarisha usalama wa nchi hiyo na pia kuathiri juhudi za kuyanyang'anya silaha vikundi vya waasi.

Miezi sita sasa imepita tangu rais huyo alipoibuka mshindi katika uchaguzi wa rais nchini humo.

Rais TOUADERA wakati anaapishwa miezi sita iliyopita alisema atatoa kipaumbele katika masuala ya usalama pamoja na kuwanyang’anya silaha waasi nchini humo.

October 10, 2016

MARTHA NGWIRA

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI