Madaktari katika hospitali za serikali SUDAN wagoma
Madaktari katika hospitali za serikali ya SUDAN wamegoma wakidai kupatiwa vifaa bora vya kufanyia kazi, nyongeza za mishahara na kuhakikishiwa usalama wao

Kamati ya shirikisho la vyama vya madaktari nchini humo imesema madaktari katika hospitali za serikali kwa sasa wanatoa huduma ya dharura tu kufuatia mgomo wao waliounza jana asubuhi.

Madaktari hao wamegoma kutokana na kulipwa mishahara midogo, kuzorota kwa huduma kwa sababu ya kutokuwepo kwa vifaa na kuongezeka kwa mashambulio yanayofanywa dhidi yao na majeshi ya usalama  pamoja na ndugu wa wagonjwa.

Katika wiki za hivi karibuni kumekuwepo na  taarifa za polisi au ndugu wa wagonjwa kushambuliwa madaktari.

 

October 7, 2016

MARTHA NGWIRA

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI